Ads 468x60px


Utalingolo,njombe,tanzania.

Friday, October 4, 2013

KUMEKUCHA UJENZI WA SEKONDARI MPYA KATA YA UTALINGOLO.

Wananchi wa kata ya Utalingolo wamefanya maamuzi  mazito ya kujenga SEKONDARI yao ya Kata,
Mnamo Tarehe 20/09/2013 Kamati ya Maendeleo ya Kata(KAMAKA) Ilikabidhiwa eneo lenye ukubwa wa ekari 30. Mnamo tarehe 23/09/2013 Halmashauri ya Mji Njombe ilimtuma afisa mipango miji kwenda kupima eneo hilo ili Mchoro(Layout) ya eneo hilo ifanyike  mapema .Hatimaye itaandaliwa michoro ya majengo ya SEKONDARI.

 
Eneo hili lipo katika kitongoji cha IGOMA kijiji cha UTALINGOLO.

  
Wananchi pamoja na viongozi wakiwa katika Eneo la ujenzi wa SEKONDARI,
kutoka kushoto:-Itine Mpete(Mwananchi),Bernard Mligo(Shahidi)Mjumbe kamati ya ujenzi wa Sekondari,Petro Mahenge(Mwenyekiti wa kitongoji na ujenzi wa Sekondari),
Mh.Bonaventura Fwalo - Diwani, Ndugu Wawason- Afisa mipango miji Halmashauri ya mji Njombe.
 


 

2 comments:

Anonymous said...

Hongereni

Anonymous said...

nawatakia ufanisi mwema maana hapo yanatakiwa maneno kidogo kazi zaidi

Post a Comment