Ads 468x60px


Utalingolo,njombe,tanzania.

Featured Posts

Sunday, May 4, 2014

WANANCHI KATA UTALINGOLO WAANZA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI









WAZEE WA KATA YA UTALINGOLO WAKISHIRIKIKATIKA UJENZI WA SEKONDARI(akitoamaoni)



















DIWANI KATA YA UTALINGOLO BONAVENTURA FWALO AKISHIRIKIANA NA WANANCHI KUCHIMBA MSINGI


TAKRIBANI MILIONI SITINI ZINATARAJIWA KUTUMIKA KWA UJENZI WA MADARASA  NA OFISI MBALIMBALI ZA SHULE HIYO AMBAYO INAENDELEA KUJENGWA KWA SASA.

Monday, March 31, 2014

UJENZI SEKONDARI YA UTALINGOLO WAANZA RASMI LEO

 Kutoka kushoto ni Berhard Mligo Mjumbe wa kamati ya ujenzi sekondari,Seraphine Msemwa ambaye nii fundi toka kampuni ya Matokeo,Paternus Mligo(Pulundu) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi,Angelus Fungiwa Makamu Sekondari ya Uwemba,Abbas Sanga Mkuu wa Sekondari Uwemba na mhasibu wa Utalingolo Sekondari,Anold Mwanyika Architect,Eng.John Kawogo Kaimu Mhandisi Halmashauri Mji Njombe na Mh.Bonaventura Fwalo Diwani wa Kata ya Utalingolo
 Kazi ya upimaji inaendelea kama wahusika wanavyoonekana................!
 Hawa ni Ndg.Paternus Mligo na Angelus Fungilwa
Kushoto ni Mkuu wa Sekondari ya Uwemba ambaye ndiye msimamizi na mhasibu wa sekondari ya Utalingolo akiwa anaangalia vipimo kama vinakwenda sawa.Katikati ni Ndg Anold E.Mwanyika .Anayefuatia ni Ndg.Abbas SangaMakamu Mkuu wa Sekondari ya Uwemba ambaye alimsindikiza mkuu wake.Wa mwisho kulia ni Eng.John Kawogo Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe ambaye alikuja kutoa maelekezo ya kitaalamu kwa mafundi ili kazi ziweze kuanza rasmi.

Wednesday, March 26, 2014

BARABARA YA NZENGELENDETE-UTALINGOLO KUFANYIWA MATENGENEZO MAALUM


Halmashauri ya Mji wa Njombe inatarajia kuifanyia matengenezo maalum barabara hii kwa kiwango cha kifusi barabara yote(FULL GRAVEL) katika fedha zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2013/2014 kiasi cha tshs.250,000,000.00(milioni mia mbili na hamsini tu).Barabara itakuwa na ubora mkubwa.Wananchi watapata fursa ya kufanya biashara na huduma zingine vizuri na kwa wakati.........................!!!!!!!!

MRADI WA MAJI LUGENGE-KISILO-UTALINGOLO WAIVA


HILI HAPA NI BANGO LA MRADI






Tanki hili limejengwa katika kijiji cha Lugenge ambako mradi unampita kutoka Ludodolelo.katika picha ni;Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Utalingolo Bw.Stanley Mgohele.Katikati ni:Mwenyekiti wa Kijiji cha Utalingolo Bw.Dominikus Njawike.Anayefuata ni Isaya Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Maji Kijiji cha Utalingolo.Wote hawa walikuja hapo siku ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh.Asery Msangi.



Huyu mama anaitwa Christina Mbena ambaye ni mjumbe wa kamati ya maji ya kijiji cha Utalingolo.Alikuwa hapo siku ya ziara ya mkuu wa mkoa wa Njombe Mh.Asery Msangi
Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Utalingolo ndg.Nolasco Mlyuka,Mwenyekiti wa kijiji cha Utalingolo ndg.Dominikus Njawike,Christina Mbena,Isaya Msigwa,Afisa Mtendaji wa Kata Ndg.Mgohele na Mh.Bonaventura Fwalo Diwani wa Kata ya Utalingolo.Hawa wote walikuja kushiriki ziara ya mkuu wa mkoa wa njombe mh.Asery Msangi

ZAHANATI YA UTALINGOLO KATIKA UKARABATI


Wananchi kwa kushirikiana na serikali wamefaulu kujenga zahanati hii na ni matarajio yao mwaka huu 2014 itakuwa imekamilika na kuanza kutumika.Wote walioshiriki kwa namna ile au nyingine wanapewa nafasi kuwa ya kupewa shukrani za pekee kwani wamefanya utekelezaji wa ilani ya ccm ya kuwafikia wananchi wake kwa kuanzisha programu ya MMAM (Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi).Kwa kuzingatia hilo serikali  katika zahanati hii imetoa vifaa vya umaliziaji vyenye thamani ya Tshs.10,000,000.00 (milioni kumi tu).Serikali ishukuriwe katika hili !

Monday, March 24, 2014

Monday, January 13, 2014

UJENZI WA MADARASA YA SHULE YA MSINGI UTALINGOLO WAPAMBA MOTO


Anayeonekana hapo ni Mh.Coleta Nyigu,diwani wa viti maalum Tarafa ya Igominyi ambaye alifika kutembelea na kukagua shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa.Kimsingi Mheshimiwa huyu amesoma shule hii !




Huyu ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Utalingolo Ndg.Chao


Huyu ni ndg Deusdedit Ngole(Hamis) mjumbe wa serikali ya kijiji cha Mfereke yupo katika shughuli za kusimamia ujenzi wa zahanati ya Mfereke.


Huyu ni Ndg.Alex Ngole ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mfereke.Yupo kikazi zaidi.Yeye ana Maneno kidogo Kazi Zaidi !

Friday, October 4, 2013

KUMEKUCHA UJENZI WA SEKONDARI MPYA KATA YA UTALINGOLO.

Wananchi wa kata ya Utalingolo wamefanya maamuzi  mazito ya kujenga SEKONDARI yao ya Kata,
Mnamo Tarehe 20/09/2013 Kamati ya Maendeleo ya Kata(KAMAKA) Ilikabidhiwa eneo lenye ukubwa wa ekari 30. Mnamo tarehe 23/09/2013 Halmashauri ya Mji Njombe ilimtuma afisa mipango miji kwenda kupima eneo hilo ili Mchoro(Layout) ya eneo hilo ifanyike  mapema .Hatimaye itaandaliwa michoro ya majengo ya SEKONDARI.

 
Eneo hili lipo katika kitongoji cha IGOMA kijiji cha UTALINGOLO.

  
Wananchi pamoja na viongozi wakiwa katika Eneo la ujenzi wa SEKONDARI,
kutoka kushoto:-Itine Mpete(Mwananchi),Bernard Mligo(Shahidi)Mjumbe kamati ya ujenzi wa Sekondari,Petro Mahenge(Mwenyekiti wa kitongoji na ujenzi wa Sekondari),
Mh.Bonaventura Fwalo - Diwani, Ndugu Wawason- Afisa mipango miji Halmashauri ya mji Njombe.